Uturuki yatangaza hali ya hatari

Rais wa Uturuki, Recep Erdogan ametangaza hali ya hatari kwa miezi mitatu katika majimbo 10 yaliyoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi lililotokea Februari 6, 2023.

Erdogan amesema idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea kusini mashariki mwa Uturuki iliongezeka hadi 3,549, na kufanya jumla ya waliouawa, wakiwemo wale wa kaskazini mwa Syria, kufikia zaidi ya 5,000.

Imeelezwa kuwa baadhi ya nchi kutoka duniani kote zimeahidi msaada katika shughuli za utafutaji na uokoaji ambazo zinatatizwa na baridi na theluji. Viongozi mbalimbali wanaendelea kujitokeza kutoa msaada wao na rambirambi.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amempigia simu Rais wa Uturuki, Erdogan kueleza masikitiko yake kwa vifo vya maelfu ya watu na kuwatakia ahueni waliojeruhiwa, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki ilisema katika taarifa yake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pia aliwasilisha salamu za rambirambi kwa Erdogan.

Wakati huo huo, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alizungumza na Bashar al-Assad wa Syria akitoa uungaji mkono kwa juhudi za misaada ya tetemeko la ardhi, rais wa Misri amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button