Uturuki yawakamata waandamanaji 42

UTURUKI : SERIKALI nchini Uturuki inawashikilia watu 42 baada ya kuwakamata kufuatia maandamano makubwa yaliofanyika mjini Istanbul, siku 100 tangu alipoondolewa na kukamatwa kwa aliyekuwa meya wa mji huo Ekrem Imamoglu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki aliandika katika mtandao wake wa X kwamba watu hao 42 wanashutumiwa kumtusi rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kushindana na maafisa wa usalama.
Maelfu ya watu waliandamana mjini humo kumuunga mkono meya Imamoglu ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya upinzani dhidi ya serikali. SOMA: Tanzania, Uturuki kushirikiana utalii
Ekrem Imamoglu ni mwanasiasa mashuhuri nchini Uturuki anayekiongoza chama kikubwa cha upinzani cha CHP na anaangaliwa kama mpinzani mkubwa wa rais Erdogan katika chaguzi zijazo.



