UVCCM Kagera yaja kivingine

KAGERA; UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kagera, umezindua kampeni ya siku 16 maarufu kama SANEVO.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan inakutanisha vijana wote bila kujali ni wanachama wa CCM au la, lengo likiwa ni kutoa elimu ya mpiga kura na kuelezea mambo mazuri yanayofanywa na serikali kwa vijana.

Kampeni hiyo imeanza Wilaya ya Karagwe, ambapo kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kagera imekutana na baadhi ya vijana ukumbi wa CCM uliopo Kayanga, wilayani Karagwe, mkoani Kagera .

Amesema pamoja na mambo mengine, pia kampeni hiyo itaangalia miradi kadhaa iliyotekelezwa wilayani Karagwe na kwamba wanatamani Mkoa wa Kagera wakati wa kampeni ukifika ufanye vizuri katika kura kwa mgombea wa urais Dk Samia Suluhu Hassan kupata ushindi wa kishindo.

“Tunatamani sana mkoa wetu upate heshima ya kuongoza kwenye kura za Dk Samia Suluhu Hassani, lakini nyinyi kama Wanakaragwe wekeni malengo ya kusema kura za nhi nzima  au za majimbo Karagwe iwe ya kwanza katika kupiga kura za Rais Samia,”amesema Faris na kuongeza kuwa kampeni hiyo itapitia wilaya zote mkoani humo.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button