Uvuvi haramu waondoka na Kaimu Mkurugenzi Uvuvi

DAR ES SALAAM; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameelekeza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Waziri Ulega ametoa maamuzi hayo wakati akikabidhi boti (11) zenye thamani ya Sh bilioni 1.85 zilizotolewa na  na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam Novemba 28, 2023.

Aidha,Waziri Ulega amefika maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi mkoani Dar es Salaam ya kukithiri kwa vitendo vya Uvuvi haramu katika ukanda wa Pwani hususani Dar es Salaam.

Advertisement

Oktoba 4, 2023 akiwa mkoani Mwanza katika Soko la Lumumba, Waziri Ulega alimtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kuwa ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Kufuatia kushindwa kutekeleza mikakati hiyo, Waziri Ulega ameamua kumuondoa katika nafasi hiyo na kuelekeza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh.

2 comments

Comments are closed.