Uwezeshaji wa rasilimali unavyoongeza ujumuishaji wa kifedha

JUHUDI za kupanua ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania zinaendelea kuimarika huku serikali na wadau wa sekta ya fedha wakitafuta njia mbalimbali za kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaofanya shughuli zao katika sekta isiyo rasmi.

Hatua hizi zinaonekana kuwa muhimu katika kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kunufaika na huduma rasmi za kifedha.

Kwa mujibu wa ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina zaidi ya watu milioni 60, huku takribani asilimia 80 ya nguvu kazi ikijihusisha na shughuli za sekta isiyo rasmi.

Sekta hii inajumuisha wafanyabiashara wadogo, waendesha bodaboda, wamiliki wa bajaji, wauza bidhaa sokoni na watoa huduma mbalimbali mijini na vijijini. Hata hivyo, wadau wa masuala ya uchumi wanasema pamoja na mchango mkubwa wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa taifa na kutoa ajira kwa mamilioni ya wananchi, bado wengi wa wanaofanya kazi katika sekta hiyo wanakumbana na changamoto ya kupata huduma rasmi za kifedha, hususani mikopo kutoka taasisi za fedha.

Changamoto hizo mara nyingi hutokana na ukosefu wa dhamana zinazotakiwa na benki, historia ya mikopo, pamoja na nyaraka rasmi za kifedha ambazo hutumika kuthibitisha uwezo wa mkopaji kurejesha mkopo.

Kutokana na hali hiyo, sehemu kubwa ya wananchi hujikuta wakitegemea mikopo isiyo rasmi au akiba za vikundi vidogo vya kijamii ambavyo mara nyingi vina uwezo mdogo wa kusaidia uwekezaji mkubwa katika shughuli za uzalishaji.

Katika miaka ya hivi karibuni, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kusisitiza umuhimu wa ujumuishaji wa kifedha kama sehemu ya juhudi za kuimarisha ushiriki wa wananchi katika uchumi rasmi kupitia mikakati ya kitaifa ya ujumuishaji wa kifedha na kuimarika kwa huduma za fedha za kidijiti.

Lengo ni kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma za akiba, malipo na mikopo kwa njia salama, nafuu na inayopatikana kwa urahisi zaidi.

Kuongezeka kwa matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu kumesababisha mabadiliko makubwa katika mfumo wa kifedha. Kupitia huduma za fedha kwa simu, mamilioni ya Watanzania sasa wana uwezo wa kutuma na kupokea fedha, kulipia huduma mbalimbali, na hata kuweka akiba bila kulazimika kutembelea matawi ya benki.

Teknolojia hii imekuwa kichocheo muhimu katika kupunguza umbali kati ya wananchi na huduma rasmi za kifedha, hasa kwa wale wanaoishi maeneo ya mbali na huduma za benki.

Hata hivyo, pamoja na maendeleo hayo katika malipo na miamala ya kidijitali, wadau wa sekta ya fedha wanasema bado kuna haja ya kupanua upatikanaji wa mikopo inayoweza kusaidia wananchi kuwekeza katika shughuli zinazozalisha kipato.

Wataalamu wa uchumi wanaeleza kuwa ujumuishaji wa kifedha hauishii tu katika kuwezesha miamala ya fedha, bali pia katika kuwasaidia wananchi kupata rasilimali zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji na kukuza biashara zao.

Katika mazingira hayo, mifumo ya ufadhili wa mali imeanza kuonekana kama moja ya njia mbadala zinazoweza kusaidia wananchi wengi zaidi kupata zana muhimu za kufanya kazi.

Mfumo huu unamwezesha mteja kupata mali ya uzalishaji kama vile pikipiki, bajaji, au simu janja kwa mfumo wa malipo ya awamu. Mali hizo hutumika moja kwa moja katika shughuli za uzalishaji na hivyo kumwezesha mteja kujiingizia kipato kitakachomwezesha kurejesha mkopo taratibu.

Katika sekta ya usafiri kwa mfano, pikipiki na bajaji zimekuwa nyenzo muhimu katika kutoa huduma hiyo kwa abiria na mizigo katika maeneo mengi ya nchi.

Watu wengi wanaojihusisha na shughuli hizi hutegemea vyombo hivyo kama chanzo kikuu cha kipato hivyo upatikanaji wa ufadhili wa mali unaweza kuwasaidia watu wengi kuingia katika shughuli hizo bila kuwa na mtaji mkubwa wa kuanzia.

Miongoni mwa wadau wanaojishughulisha na utekelezaji wa mfumo wa ufadhili wa mali ni Taasisi ya Watu Tanzania.

Hivi karibuni taasisi hiyo iliandaa futari mkoani Dar es Salaam na kukutanisha waandishi wa habari ili kujadili mchango wa huduma hiyo katika kuboresha fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Hafla hiyo ilitoa nafasi kwa wadau mbalimbali kuelezea uzoefu wao kuhusu namna mifumo ya ufadhili wa mali inavyoweza kusaidia kupunguza pengo la upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa katika hafla hiyo, zaidi ya wateja milioni 1.05 Tanzania wamepata mali za uzalishaji kupitia mifumo ya ufadhili wa mali tangu huduma hizo zilipoanza kutolewa mwaka 2021. Inakadiriwa kuwa zaidi ya familia milioni 3.1 zimenufaika moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia wanufaika wa ufadhili huo.

Akizungumza katika mjadala huo, Meneja Mkazi wa Watu Tanzania, Rumisho Shikonyi, anasema upatikanaji wa mali za uzalishaji unaweza kusaidia kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wengi, hasa wale wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi.

“Upatikanaji wa zana zinazowezesha watu kufanya kazi unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi. Watu wanapopata mali zinazowawezesha kufanya shughuli za kiuchumi, wanapata fursa ya kuongeza kipato na kuboresha ustawi wa familia zao,” anasema.

Tafiti mbalimbali pia zinaonesha kuwa huduma za ufadhili wa mali zinaweza kusaidia kuboresha kipato cha wananchi. Tafiti zilizotajwa katika hafla hiyo zinaonesha kuwa baadhi ya wateja wameongeza kipato chao kwa kati ya asilimia 50 hadi 64 baada ya kupata mali za uzalishaji. Hii inaonesha kuwa upatikanaji wa rasilimali sahihi unaweza kuwa na athari kubwa katika uwezo wa wananchi kujitegemea kiuchumi.

Utafiti wa GeoPoll wa mwaka 2024 pia unaonesha kuwa kati ya asilimia 30 hadi 57 ya watu waliopata ufadhili wa mali waliripoti kupata fursa mpya za kiuchumi. Baadhi yao walipanua biashara, wengine walianzisha shughuli mpya za uzalishaji ambazo awali hawakuweza kuanzisha kutokana na ukosefu wa mtaji.

Kwa upande wake Naibu Meneja Mkazi wa Watu Tanzania anayesimamia Mikopo, Edsteve Mwangalimi, anasema upatikanaji wa mikopo inayowezesha uwekezaji katika mali za uzalishaji unaweza kuwa sehemu muhimu ya kuimarisha ujumuishaji wa kifedha nchini.

“Upatikanaji wa mikopo inayolenga shughuli za uzalishaji unaweza kuwasaidia wananchi kujenga vyanzo endelevu vya kipato na kuboresha ustawi wa familia zao,” anasema.

Kadiri Tanzania inavyoendelea kuimarisha juhudi za kuongeza ujumuishaji wa kifedha na matumizi ya teknolojia katika huduma za kifedha, wadau wa sekta hiyo wanasema kuwa ushirikiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi utaendelea kuwa muhimu.

Ushirikiano huo unaweza kusaidia kubuni mifumo mipya ya kifedha inayolenga mahitaji ya wananchi wa kipato cha chini na wale wanaofanya kazi katika sekta isiyo rasmi.

Kwa mtazamo wa muda mrefu, wataalamu wa uchumi wanaamini kuimarika kwa mifumo ya ufadhili wa mali na maendeleo ya teknolojia ya fedha, kunaweza kuwa nyenzo muhimu katika kupunguza pengo la kifedha na kuongeza ushiriki wa wananchi katika uchumi wa taifa.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. MAWAZO YA KIONGOZI KAZI - HAUKUOA MKE SAHIHI SIWEZI KUKUBALI MUWE MWILI MMOJA - BORA MUWE NA MWILI MMOJA NA GARI YA TAKATAKA says:

    ### **TANGAZO LA AJIRA**

    **KAMPUNI YA WAJA YA BUZA**
    Inatangaza nafasi za ajira kwa wahariri wa vitabu.

    #### **Nafasi: Mhariri wa Kitabu cha Wanandoa**

    **Kitabu kinachohaririwa:**
    *“HAUKUOA MKE SAHIHI SIWEZI KUKUBALI MUWE MWILI MMOJA – BORA MUWE NA MWILI MMOJA NA GARI YA TAKATAKA”*
    Kilichoandaliwa na **Kampuni ya Waja Ya Buza**.

    **Maelezo ya Kazi:**
    Kampuni ya Waja Ya Buza inatafuta wahariri wenye ufanisi na uzoefu kwa ajili ya kuhariri kitabu cha wanandoa kinachozungumzia masuala ya ndoa, mahusiano, na changamoto zinazokutana na wanandoa. Kitabu hiki kinalenga kuleta mjadala kuhusu umoja katika ndoa na maadili ya kijamii, na kinahitaji mhariri ambaye ataweza kuboresha maandiko ya kitabu hicho kwa namna inayovutia na inayoeleweka.

    **Majukumu:**

    * Kurekebisha na kuhariri maandiko ya kitabu ili kuzingatia ubora wa kiandishi, sarufi, na mtindo.
    * Kuhakikisha kwamba ujumbe wa kitabu unafikika kwa wasomi na umma kwa ujumla.
    * Kutoa mapendekezo ya kuboresha yaliyomo ili liwe na manufaa kwa jamii, hasa kwa wanandoa na watu wanaozungumzia mahusiano.

    **Mahitaji:**

    * Uzoefu wa angalau miaka 2 katika kuhariri vitabu, makala, au maandiko yanayohusiana na masuala ya kijamii na mahusiano.
    * Uwezo wa kuelewa na kuchambua mada nzito zinazohusiana na ndoa na familia.
    * Ufanisi katika kutumia mbinu za kisasa za uhariri na kuandika.
    * Uwezo wa kufanya kazi kwa karibu na waandishi na wateja wengine ili kufanikisha mabadiliko ya kitaalamu.

    **Maslahi:**

    * Malipo ya ushindani kulingana na uzoefu na kiwango cha kazi.
    * Fursa ya kushiriki katika mradi wa kipekee wenye athari kubwa kwa jamii.

    **Jinsi ya Kuomba:**
    Waombaji wanatakiwa kutuma barua ya maombi pamoja na CV na mfano wa kazi za awali (kama zipo) kwa anwani ya **[email]** au kwa kutumia njia ya mtandao kwenye **[website]**.

    **Tarehe ya Mwisho ya Kuomba:**
    **[23/3/5000]**

  2. MAWAZO YA KIONGOZI KAZI - HAUKUOA MKE SAHIHI SIWEZI KUKUBALI MUWE MWILI MMOJA - BORA MUWE NA MWILI MMOJA NA GARI YA TAKATAKA says:

    —.

  3. MAWAZO YA KIONGOZI KAZI - HAUKUOA MKE SAHIHI SIWEZI KUKUBALI MUWE MWILI MMOJA - BORA MUWE NA MWILI MMOJA NA GARI YA TAKATAKA says:

    —;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button