Uzalishaji maziwa waongezeka nchini

MOROGORO: BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imesema kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 3.97 kwa mwaka 2023/2024 hadi kufikia lita bilioni 4.01 mwaka 2024/2025.
Ofisa wa Teknolojia ya Chakula wa Bodi hiyo,Rajilan Hilali amesema hayo kabla ya kukaribishwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa yatakayofanyika mkoani humo kuanzia Mei 27 hadi Juni 1.
Maadhimisho hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro na Kauli mbiu ya mwaka huu (2025): “Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu”.
Hilali amesema TDB iliweka mikakati endelevu ya uzalishaji wa maziwa na kuweza kufanikiwa ambapo kwa mwaka 2024/2025, uzalishaji umefikia lita bilioni 4.01 kutoka kwa ng’ombe milioni 39 waliopo nchini.
Amesema bodi imeweza kufikia kwa hatua hizo licha ya kwamba bado kuna changamoto ya uzalishaji wa maziwa kutokana na aina ya mifugo inayofugwa, hasa mifugo ya kienyeji.
“Kuna fursa kubwa kwa wafugaji, na masoko yapo Afrika, hili jambo la kuongeza uzalishaji wa maziwa linaendana na mkakati wa kuelimishana, ni lazima tuweke mikakati,” amesema Hilali.
Hilali pia amesema upatikanaji wa maziwa katika ukanda wa kitropiki wenye joto kubwa kunafanya uzalishaji maziwa kuwa na changamoto ya upatikanaji wa maziwa kwa kiwango kidogo.
Amesema kutokana na mazingira ya hali hiyo, wafugaji wanashauriwa kufunga ng’ombe aina ya chotara ili wawawezeshe kupata walau wastani wa lita 10 hadi 15 za maziwa kwa siku.
“Kwa mfano mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ndo unaweza kupata maziwa lita 20 kutokana na ukanda wa hali ya hewa kuwa baridi,”amesema Hilali.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Msajili wa Bodi hiyo, Said Isike amesema wanafunzi 89,922 kutoka shule 140 zipo halmashauri za wilaya kutoka mikoa 10 ya Tanzania Bara wananufika na mpango huo.
Isike ambaye pia ni Ofisa Masoko wa Bodi amesema halmashauri zenye shule hizo ni ya mikoa ya Kilimnjaro, Tanga, Arusha, Iringa, Mbeya, Njombe, Mwanza , Mara na Morogoro .
Ofisa Masoko wa Bodi hiyo amesema mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari utakuwa ni endelevu katika shule zingine kwenye halmashauri za wilaya nchini.
“ Mpango huu utakuwa endelevu katika halmashauri zingine nchini lakini kwa sasa utatekelezwa kwenye shule 140 miongoni mwa hizo mbili ya Mafiga na Mchikichini za Manispaa ya Morogoro , kuna vibanda vya kampuni mbalimbali vimewekwa maziwa na wanafunzi wanapata kwa bei nafuu “ amesema Isike .
Ofisa Masoko wa Bodi ya Maziwa amesema lengo kubwa la mpango huo ni kujenga tabia ya wanafunzi kunywa maziwa kwani.