Vifo ajali Kenya vyafikia 51

IDADI ya waliofariki katika ajali ya gari makutano ya barabara ya Londiani nchini Kenya imefikia 51.

Ajali hiyo imetokea Juni 30, 2023 baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuyaparamia magari mengine pamoja na watembea kwa miguu.

Polisi imesema ajali hiyo imetokea kwenye barabara inayounganisha miji miwili ya Kericho na Nakuru, hata hivyo maafisa usalama wamesema mbali ya vifo hivyo watu wengine 30 wamejeruhiwa na kupelekewa.

Rais wa Kenya, William Ruto ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa Kaunti ya Kericho anasema jumla ya miili 51 imepokelewa katika Hospitali ya Kaunti ya Kericho na hifadhi za maiti za Hospitali ya Londiani, mpaka leo asubuhi.

Habari Zifananazo

Back to top button