Vifo vya kimbunga Chido vyafikia 45

MSUMBIJI : IDADI ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia 45, baada ya kimbunga hicho kupiga mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa nchi.

Taasisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Majanga nchini Msumbiji imetangaza kuwa watu 38 wamepoteza maisha katika mkoa wa Cabo Delgado, huku wanne wakithibitishwa kufariki katika mkoa wa Nampula na watatu katika mkoa wa Niassa.

Taarifa za awali zilionyesha vifo 34, lakini hali imeendelea kuwa mbaya huku  nyumba 24,000 zimeharibiwa  na nyingine 12,300 zimeharibika kwa kiwango kidogo.

Advertisement

Zaidi ya watu 181,000 wameathirika na kimbunga hicho, huku serikali ikiendelea na juhudi za kutoa msaada na kurejesha hali ya kawaida. SOMA: WB yatoa Dola milioni 150 kimbunga freddy Msumbiji