Vijana sanaa ya uchongaji waomba msaada wa serikali

VIJANA wanaojishughulisha na sanaa ya uchongaji wa bidhaa mbalimbali mkoani Mtwara ikiwemo vinyago wameiomba serikali kuwashika mkono ili waweze kukuza na kuongeza ubunifu .

Wazo hilo limetolewa na vijana hao wakati wa mafunzo ya siku 24 kwa vijana hao yaliyoandaliwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya sanaa na utamaduni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani (ADEA) iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Andrea Njudi kutoka Kijiji cha Litembe Kata ya Madimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili vijana hao ni kukosekana kwa soko la bidhaa hizo hali inayopelekea kukata tamaa ya kujishughulisha na biashara hiyo.

“Kutokana na hii changamoto hata asili ya Mtwara sasa inapotea kwa kukosekana wachongaji kama ambavyo kipindi cha nyuma ilivyokuwa na uwezo wa kufanya hii kazi tunao mkubwa sana ila changamoto inakuja hapo kukosekana kwa soko,”amesema Njudi.

Ameongeza kuwa: “Kukosekana kwa soko la bidhaa za uchongaji ni kutokana na serikali kutotilia mkazo jambo hili na hii inaingia ugumu hata kizazi kipya wanashindwa kuingia kwenye sanaa hii kwakuona haina manufaa kwa watu hususani wanaowazunguka kwahiyo tunaiomba serikali kutusaidia sisi vijana katika hili ili tuweze kujiajiri”.

Mkazi wa Manispaa hiyo, Seif Mohamed ameiomba serikali kwa kushirikiana na ADEA kutilia mkazo elimu na sayansi inayohusu mambo ya asili ili kukuza sanaa na utamaduni wa Mtwara kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye lakini taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Saidi Chilumba amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa vijana hao elimu itayowasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora zitazoendana na wateja hasa wanaotoka nje ya nchi pia kutangaza huduma na bidhaa hizo zitazozalishwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button