Vijana wahitajika maonesho ya ubunifu

SHINYANGA: WAJASIRIAMALI 600 nchini wanatarajiwa kuonesha bidhaa zao mpya za ubunifu,kubadilishana ubora na kuuza huku vijana wanaochipukia wakiombwa kuhudhuria kujifunza zaidi kwa kile walichonacho ili kujiajiri na kunyanyua vipato vyao.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda (SIDO), Mhandisi poresa Slyvester Mpanduji kwenye hafla fupi ya kutambulisha maonesho ya tano kitaifa yatakayofanyika mkoani Shinyanga Oktoba 21- 31, 2026 Manispaa ya Kahama.
Profesa Mpanduji amesema maonesho hayo wajasiriamli watapata fursa ya kujifunza na kuongeza wigo wa kuuza na kutambulisha bidhaa wanazozalisha hata nje ya nchi kupitia washiriki 600 na taasisi 50 kushiriki kutoka kote Tanzania Bara na Zanzibar.
Profesa Mpanduji amesema kupitia maonesho hayo watatarajia wajasiriamali wa viwando vidogo na kati kujifunza mbinu mpya za uzalishaji na biashara kuingia kwenye ushindani wa ubora wa bidhaa na kuingia kwenye uwekezaji kwa taasisi binafsi na serikali pia vijana wajasiriamali watapewa kipaumbele kwa bidhaa wanazo zalisha.

Ofisa Rasilimali Watu Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akiongea kwa niaba ya katibu tawala Salum Hamduni amesema maonesho hayo yatafanyika Manispaa ya Kahama huku akieleza eneo hilo ni kitovu cha biashara na muingiliano wa watu wengi na miundombinu ya usafiri kutoka kila pembe ya mji upo vizuri ila wajasiriamali ndani ya mkoa watumie fursa hii waone nakujifunza..
Kaimu Meneja Mkoa wa Shirika la Sido, Ally Mtware amesema wajasirimali wote wajitokeze waweze kutafuta masoko na wale wanaoanza wajifunze hivyo wameandaa mafunzo rasmi kwaajili ya vijana wajifunze na kuna mfuko maalum kupitia Benki ya NMB unao wakopesha.
Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi Kambasi (kizumbi) John Mwera amesema wamekuwa wakihakikisha wanawasaidia vijana waliopo chuoni na kuwafundisha mbinu mbalimbali za kujiimarisha kiuchumi na sasa wapo kwenye ushindani wa teknolojia .



