Vijana watatu raia wa Ufaransa waachia na Hamas

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna amesema vijana watatu raia wa Ufaransa ni miongoni mwa mateka walioachiliwa na Hamas siku ya Jumatatu na kuongeza kuwa walikuwa na afya njema.


Tuna habari zisizo za moja kwa moja, na habari hizo ni nzuri … ni faraja kubwa,” Colonna aliiambia redio ya RTL, alipoulizwa kuhusu afya ya Eitan, 12, Erez, 12 na Sahar, 16.

“Watoto watatu wa Ufaransa waliachiliwa hatimaye; sasa lazima tufanye kazi bila kuchoka ili kuachiliwa kwa mateka wengine wote,” alisema, akiongeza kuwa raia watano wa Ufaransa bado hawajapatikana au wanaaminika kuwa wamefungwa.

Advertisement
4 comments

Comments are closed.