Vijiji 66 Kigoma vyaungwa gridi ya taifa

KIGOMA: Jumla ya kaya 1800 katika vijiji 66 mkoani Kigoma zimeunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa kupitia mpango wa umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vjijini (REA) ikiwa ni kutekeleza mpango wa serikali wa kuinua uchumi wa wananchi vijijini.

Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya TANESCO inayojishughulisha na ujenzi, ukarabati na uwekaji wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme(ETDCO) inayotekeleza mradi wa umeme vijijini mkoa Kigoma, Richard Mwanja amesema hayo wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Raymond Mbilinyi na wajumbe wa bodi hiyo walipofanya ziara kutembelea mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na Kampuni hiyo mkoani Kigoma.
Mwanja amesema kuwa jumla ya kaya 2200 zimepangwa kufikishiwa umeme vijijini kwa ajili ya matumizi ya majumbani katika Mkoa Kigoma ambapo kiasi cha Sh Bilioni 10.5 zinatarajia kutumika kwenye utekelezaji huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.

Meneja huyo alibainisha kuwa wateja wakubwa wanaotumia umeme wa viwandani 22 wameunganishiwa umeme kati ya lengo la wateja 55 huku transforma 51 zikiwa zimefungwa kati ya lengo la kufunga transforma 59 huku kasi ya wateja wa majumbani kuunganishwa umeme ikiwa ndogo.
Akizungumza kwenye ukaguzi huo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya ETCDO, Raymond Mbilinyi amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kujitokeza kuweka umeme kwenye maeneo yao kwani serikali kupitia REA imechangia gharama kubwa hivyo mwananchi anapaswa kulipa shilingi 27,000 kuweza kupata umeme huo ili kuchochea shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kaseke wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, Angalienni Phares ameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuwezesha umeme kufika vijijini na kila mwananchi kuweka umeme kwa gharama nafuu jambo ambalo litachochea sbuguli za uchumi na uzalishaji vijijini.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site