TETESI za usajili zinasema Aston Villa ipo tayari kushindana na Barcelona na Chelsea kumsajili mchezaji nyota wa Hispania Nico Williams, ambaye alikubalika kwa mara ya kwanza kwa kocha Unai Emery majira ya kiangazi yaliyopita.
Nico Williams, aliyezaliwa Julai 12, 2002, huko Pamplona, Hispania, ni anakikipiga kama winga wa Athletic Bilbao ya Ligi Kuu ya nchi hiyo, La Liga na timu ya taifa.
Anajulikana kwa kasi yake ya ajabu, ujuzi wa kutembea na mpira na uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga magoli.
Soma: Erling Haaland, Nico Williams kutua Barcelona
Williams alianza maisha ya mpira akiwa kinda katika klabu ya Osasuna kabla ya kuhamia kwenye kituo cha kukuza vipaji vya soka cha Athletic Bilbao mwaka 2013, ambapo alipanda haraka kutokana na kuonesho mchezo wa kuvutia.
Williams alianza kucheza katika timu ya wakubwa ya Athletic Bilbao mwezi Aprili 2021 na akajidhihirisha haraka kama mchezaji muhimu kwa timu.

Aling’aa zaidi msimu wa 2021-2022 licha ya umri wake mdogo wa miaka 20 kwa kuonesha kiwango cha juu cha uchezaji.
Katika ngazi ya kimataifa, Nico Williams aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Hispania Septemba 2022, akicheza mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya Ligi ya Mataifa ya UEFA.
Alichaguliwa kwenye kikosi cha Hispania kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 na ni mmoja wa wachezaji wa kikosi cha nchi hiyo kilichotwaa ubingwa Kombe la Mataifa ya Ulaya(EURO2024) Julai 14, 2024.

Katika tetesi nyingine Manchester City imekataa ofa ya pauni milioni 25 toka klabu ya Al Nassr kwa ajili ya kumsajili golikipa Ederson, ikisema kipa huyo raia wa Brazil ana thamani mara mbili ya kiasi hicho.(Fabrizio Romano)
Real Madrid itafanya jaribio jipya kumsajili Leny Yoro baada ya timu ya Lille kukubali ofa ya Manchester United kuhusu beki huyo.(RMC Sport – France)
Man Utd inaendelea kujadiliana vipengele binafsi na Yoro ikitumaini atabadili mawazo yake. (The Guardian)
Liverpool bado ina nia ya kumsajili kiungo wa Atalanta Teun Koopmeiners, na majogoo hao wa Anfield wako mbele ya Juventus katika mbio za kumwania nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi.(Calciomercato – Italy)