Viongozi wa dini wakataa migongano,vita

VIONGOZI wa dini ya Kikristo nchini wamewataka waumini wa dini hiyo kudumisha upendo, msamaha na kukataa migongano na vita. Wameeleza hayo katika ibada na misa za Ijumaa Kuu katika maeneo mbalimbali nchini wakisisitiza kumshukuru Mungu katika kukumbuka mateso ya Yesu Kristo. Akitoa salamu za Pasaka itakayoadhimishwa kesho duniani, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Dk Abednego Keshomshahara amehimiza kuomba na kukataa roho za vita na migongano.

“Tuendelee kuomba na tuendelee kupaza sauti na kuomba kukataa roho za vita na migongano,” alisema na kutoa mfano wa nchi mbalimbali zenye vita inayoathiri maisha ya watu wengi na kusisitiza kutokata tamaa. SOMA: Umoja Ni Nguzo ya Amani

Amesema kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kunaonesha matumaini mapya kwa wanadamu na kwamba pamoja na magumu yoyote ambayo mwanadamu anaweza kupitia, bado mambo yanaweza kubadilika kuwa mazuri. “Yawezekana hata wewe unapita katika shida katika mateso, mahangaiko na changamoto za maisha lakini usikate tamaa ushindi unakuja, ili mradi umemuamini huyo ambaye amesema “Aniaminiye mimi, ajapokufa atakuwa anaishi”,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Arusha (UKAMA), Askofu Dk Stanley Hotay amewataka Watanzania kutambua kuwa Ijumaa Kuu si tukio la kihistoria pekee, bali ni siku yenye ujumbe hai wa msamaha, upendo na mabadiliko ya maisha. Askofu Dk Hotay amesema hayo katika ibada ya pamoja ya madhehebu mbalimbali ya Kikristo iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Katoliki Mtakatifu Thereza, Jimbo Kuu la Arusha.

Akihubiri, amehimiza msamaha akisema msalaba wa Yesu Kristo una maana pana zaidi ya mateso, kwani ndiyo chanzo cha msamaha na ukombozi wa mwanadamu. Ameeleza kuwa licha ya kunyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa, Yesu alichagua kusamehe badala ya kulipiza kisasi, akitoa mfano wa hali ya juu wa uvumilivu na upendo. “Watu wengi husema wokovu ni bure lakini ukweli ni kwamba ulilipiwa gharama kubwa sana. Yesu aliteseka kwa ajili yetu akitufundisha thamani ya kusamehe,” alisema.

Aidha, amewataka Watanzania kutumia maadhimisho ya Ijumaa Kuu kujitathmini binafsi na kitaifa. Amesema jamii imejaa chuki na uhasama, hivyo suluhisho ni kusamehe na kuanza upya kwa mustakabali wa taifa. Mchungaji KKKT, Usharika wa Kimara, Wilbroad Mastai alisema Ijumaa Kuu ni siku ya kazi ya kumsifu na kumshukuru Mungu kwa kujitoa kwa ajili ya watu.

“Ijumaa Kuu ya 2026, ajenda kuu ya moyo wako isiwe kupeleka maombi, iwe ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya dhabihu inayoitwa Yesu Kristo,” alisema. Akizungumza katika adhimisho la mateso ya bwana katika Parokia ya Bunju, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Stephano Musomba alisema ni muhimu kuambizana ukweli na kwamba ili kumuelekea Mungu, ni muhimu watu wakawa wakweli, wema, wenye uzuri na umoja.

“Tukiambizana ukweli tutasonga mbele lakini kama tutasifiana tu tutapotea, hatuitakii vyema nchi yetu na hatuwatakii mema watoto na wajukuu zetu. Tukae, tujitathmini, tuambizane ukweli na tuumeze; ukweli unauma lakini utatuponya,” alisema.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Start now generating extra home based cash by doing very easy and simple job from home. Last month i have earned $19753 from this job in my part time. This job is just awesome and its earning are greater than 9 to 5 office job. Join this right now by follow instructions here…

    >>>>>>>>>> http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button