Viongozi watakiwa kueleza thamani na chanzo mali zao

MOROGORO: SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema sheria ya maadili ya viongozi wa umma inawataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wawe wazi kuorodhesha mali au rasilimali wanazomiliki.

Viongozi hao wa umma wanatakiwa pia kuelezea thamani ya mali hizo na jinsi zilivyopatikana ili kuthibitisha uhalali wa mali wanazomiliki.

Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mkuu wa Kanda ya Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Morogoro na Tanga ,Henry Sawe alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya maadili na ujazaji wa tamko kwa njia ya mtandao (ODS).

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro yaliwashirikisha viongozi waandamizi wa Serikali na Taasisi za umma , wakiwemo na maofisa Tehama wa mkoa huo.

Sawe amesema utoaji wa tamko ni takwa la kisheria na inawataka viongozi wa umma kutoa matamko yao wanapoingia madarakani ndani ya siku 30 mwisho wa mwaka pamoja na wanapoondoka kwenye nafasi za uongozi.

“Utaratibu huu upo kisheria na ni kiyume na sheria kwa kiongozi wa umma kushindwa kutoa tamko ama kuchelewa kutoa tamko kwa wakati,” amesema Sawe.

Amesema kuwa ,kuna umuhimu wa viongozi wa umma kuendelea kuimarisha dhana ya uwajibikaji na uwazi kwa  ujazaji wa tamko kwa njia ya mtandao.

Sawe amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nguvu zaidi kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi ili  kuwawezesha viongozi wote waliopo ndani na nje ya nchi kuweza kuwasilisha matamko yao kwa njia ya mtandao.

Amesema utaratibu huo unawawezesha viongozi kuwasilisha taarifa zao kwa wakati na hata kwa watumishi wa taasisi simamizi kuweza kuchakata taarifa hizo kupitia mifumo ya mtandao.

Sawe amesema  kuwasilisha taarifa hizo kwa njia hiyo kurahisisha maofisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuchakata taarifa hizo kwa urahisi na kupata matokeo yaliyokusudiwa.

“Mafunzo haya tumeanza na  mkoa wa Morogoro na yataendelea mkoa wa Tanga lengo ni  kuwafikia viongozi wa umma waliopo maeneo haya  kutoka halmashauri, taasisi na mashirika ya umma,” amesema Sawe .

Pia amesema maofisa tehama na wakuu wa vitengo wa tehama wanaopatiwa mafunzo hayo , na wao watakwenda kuwawezesha viongozi maeneo yao wakiwemo Madiwani na wakuu wa Idara kwenye halmashauri ili waweze kuufikia mfumo na kuwasilisha taarifa zao ambalo ni takwa la kisheria .

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mkoani Morogoro, Mhandisi Emmanuel Ndyamukama, ambaye ni miongoni mwa washiriki amesema ujazaji fomu za maadili kwa kutumia njia ya mtandao ni jambo la muhimu.

Mhandisi Ndyamukama amesema hatua hiyo inarahisisha utendaji kazi tofauti na miaka ya nyuma nyakati za kujaza fomu kwenye karatasi ikiwa na  kusafiri umbali mrefu kuziwasilisha kwa kamishina wa Maadili.

“Mafunzo haya yametujengea uelewa wa kujua sheria za maadili ya viongozi wa umma, na utakuwa ni zitatuongoza kwenye utekelezaji majukumu ya kila siku,” amesema Mhandisi Ndyamukama.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button