Vitanda changamoto wodi mama na mtoto hospitali Mkuranga

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, inakabiliwa na upungu mkubwa wa vitanda katika wodi ya mama na mtoto hali inayowalazimu wanawake waliojifungu kulala watu watatu katika kitanda kimoja.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Angelus Mtewa, wakati akipokea msaada wa kitanda kimoja cha kujifungulia wanawake wajawazito na baadhi ya vifaa vingine, vilivyotolewa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Pwani katika mahadhimisho ya wiki ya shukrani kwa mlipa kodi.

Advertisement

Alisema, jengo la mama na mtoto lilipo katika hospitali hiyo lina uwezo wa kuhudumia wanawake 70 kwa mwezi lakini linahudfumia wanawake zaidi ya 500 kwa mwenzi hali inayosababisha upungufu wa vitanda na baadhi ya vifaa tiba.

“Jengo letu lina uwezo wa kuhudumia wanawake 70 tu Kwa mwezi lakini tunahudumia wanawake zaidi ya 500 tofauti na mahitaji hivyo wengi wanalala watatu katika kitanda kimoja na unakuta mama amejifungua kwa upasuaji”alisema Mtewa.

Aidha alisema mahitaji ya vitanda vya kuwalaza wanawake baada ya kujifungua ni zaidi ya 50 na kwamba vilivyopo ni vitanda 18 pekee huku vitanda vya kujifungulia vikiwa nane na mahitaji yakiwa vitanda 20.

“Changamoto nyingine ni jengo letu ni dogo halitoshelezi mahitaji, wanawake wengine wanalala chini na tena wamefanyiwa upasuaji, hivyo tunaishikuru (TRA) kwa kutupatia msaada ila bado tunahitaji misaada zaidi wadau wengine wajitokeze.”alisema.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) , Mkoa wa Pwani Masawa masatu, alisema wameshereka siku hiyo ya kutoa shukrani kwa walipa kodi kwa kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 5 katika hospitali hiyo wa kitanda kimoja cha kujifungulia, magodoro 20, mashuka 50, taulo za kike pamoja na vifaa baadhi ya vifaa vingine.

“TRA tupo katika wiki ya shukurani Kwa walipa kodi wetu na siku hii yunataratibu wa kutembelea walipa kodi na wahitaji kwa ajili ya kutoa misaada…Leo tumetoa msaada wa kitanda,Magodoro na mashuka lengo letu ni kuhakikisha wamama wanajifungua salama katika mazingira rafiki.