MECHI sita za michuano ya Kombe la Carabao huko England zinapigwa leo katika vianja tofauti.
Brighton inaialika bingwa mtetezi Liverpool katika uwanja wa The American Express Community huku Crystal Palace ikiwa mgeni wa Aston Villa katika uwanja wa Villa Park.
SOMA: Majogoo watwaa Carabao kibabe
Manchester United ambayo imemtimua Erik Ten Hag hivi karibuni ni mwenyeji wa Leicester City katika uwanja wa Old Trafford.
Kipute kingine kinachosubiriwa kwa hamu ni kati ya Tottenham Hotspur na Manchester City kwenye uwanja wa Tottenham Hotspur.
Arsenal itakuwa ugenini kuivaa Preston North End kwenye uwanja wa Deepdale wakati Newcastle United ni mwenyeji wa Chelsea katika uwanja wa St James’ Park.