Vyama vinne havikuweka kwenye akaunti zao mil 31.7/-

DODOMA: MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ameeleza katika ripoti yake kuwa vyama vya siasa vinne vilikusanya Sh milioni 31.7 lakini havikuwasilisha fedha hizo katika akaunti za benki za vyama husika.

Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 iliyorekebishwa mwaka 2019, kinataka kila chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria kufungua akaunti ya benki ya chama ambayo mapato yote yanayopatikana kutokana na ada za uanachama, michango ya hiari, misaada, ruzuku, au mapato ya uwekezaji yanapaswa kuwasilishwa benki.

Katika ripoti yake, CAG imevitaja vyama hivyo kuwa ni (NCCR Mageuzi) Sh milioni 26.226 2, Chama cha Kijamii (CCK) Sh milioni 2.882, Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Sh milioni 2.175 na National League for Democracy (NLD).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button