‘Vyombo vya ulinzi na usalama viheshimiwe’

SHINYANGA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCMA), Kenani Kihongosi amewataka wananchi kuheshimu vyombo vya ulinzi na usalama, kwani wamekula kiapo cha kulilinda taifa hadi kufa.

Kihongosi ameeleza hayo Machi 6,2026 jioni wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya shule ya Msingi Town Halmashauri ya Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga, ikiwa ni ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na wnanachi hao Kihongosi amesema kila mwananchi ana wajibu wa kuheshimu vyombo vya ulinzi na usalama kwani kila mtu anapokuwa ndani kwake vyombo hivyo vinachukua jukumu la ulinzi kw akufanya doria wakiwa nje.

“Tuna wajibu wa kuheshimu vyombo vyetu maduka yale ikifika saa 1:00 jioni yote yanafungwa anayelinda maduka nani ni ninyi au askari ?,” amehoji Kihongosi.

Amewasisitiza wananchi kuwa na tabia ya kutii na kuthamini vyombo hivyo, kwani kutokufanya hivyo taifa zima litaharibika na kujikuta likiingia katika machafuko bila kutarajia.

“Leo tukisema askari wote nchi nzima waende likizo ya mwezi mmoja traffic wote watoke, vituo vyote vya polisi vifungwe, magereza na mipaka wanajeshi wote waondoke nini kitatokea maisha yatakuwa mazuri?,” alihoji.

Alisema ni lazima waheshimiwe na wapendwe kwani wamekula kiapo cha kulinda taifa hadi kufa kitu ambacho wananchi hawawezi kufanya, mida wote wamevaa sare, nidhamu, kazi, utii, amri ili kuhakikisha maisha ya wananchi yanakuwa bora.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button