Waamuzi sita watimuliwa kisa Vini Jr

SHIRIKISHO la Soka la Hispania na Kamati ya Ufundi ya Waamuzi imewatimua waamuzi sita wa VAR kufuatia kumuonesha kadi nyekundu mchezaji wa Real Madrid, Vinícius De Oliveira maarufu kama ‘Vini Jr’ huku akikutana na tuhuma za ubaguzi wa rangi.

Vinicius alikuwa sehemu ya mchezo wa La Liga kati ya Real Madrid walipopoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Valencia Jumapili.

Winga huyo wa Brazil awali alikabiliana vikali na wafuasi wa Valencia, ambao walidaiwa kumbagua Vinicius wakiwa kwenye jukwaani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kisha alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kofi Hugo Duro baada ya kuchezewa rafu na hivyo kuzua kejeli kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.

Akitumia mitandao ya kijamii baada ya mchezo huo, Vinicius alichapisha taarifa yenye nguvu ya kulaani vitendo vya wafuasi hao, na kutochukuliwa hatua kutoka kwa La Liga.

Habari Zifananazo

Back to top button