“Waandishi ifuateni Tume Huru ya Uchaguzi”

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kama kuna jambo lolote waandishi wa habari wanataka kufahamu kuhusu uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi ipo waione.
Akizungumza leo Julai 9, 2025 katika Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025 jijini Dar es Salaam, Dk Biteko amesema serikali ilifanya maboresho ya sheria ili iwe huru isiingiliwe na mtu.
SOMA ZAIDI
Sisi kama Serikali ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa waandishi wa habari katika kipindi chote cha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wanabaki salama wao pamoja na mali zao. Serikali tutaendelea kulisimamia hili kwa nguvu zetu zote,”
Waandishi wa habari mnatakiwa kuwa walinzi wa kweli, wajenzi wa amani na wachochezi huku mkiwabaini na kuwawajibisha ninyi kwa ninyi bila kisubiri vyombo vya dola. Ni wajibu wenu pia kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinabaki kuwa kioo safi cha jamii kisichokuwa na doa wala uzushi, chuki wala upendeleo,”amesema Dk Biteko.



