Waandishi wa habari wachangia damu Mtwara

KATIKA Kuandhimisha Miaka 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka 2023, waandishi wa habari Mtwara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameadhimisha siku hiyo kwa kuchangaia damu ili kuboresha hifadhi ya damu katika hospitali mbalimbali.

Akizunguma leo mkoani Mtwara katika zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha akiwa miongoni mwa waliochangia amewapongeza na kuwashukuru wanahabari hao kwa hiyari yao kwa kufanya jambo hilo.

‘’Mumetimiza wajibu wenu kufikiria suala hili la kuchangia damu kwani umuhimu wa kuchangia damu upo pale pale kwasababu bado tunafahamu damu haitengenezwi nje ya mwili wa binadamu hakuna huo utaalam mpaka sasa na uhitaji wa damu bado upo lakini pia kwa wale wanaoamini katika dini zote hili jambo lina faida hata kwa Mungu’’,Amesema Msabaha

Msabaha ameongeza kuwa, ‘’Umuhimu wa kuchangia damu ni mkubwa kutokana wagonjwa tunao wanaopata ajali mbalimbali, watoto hasa chini ya miaka mitano, akina mama wajawazito na wale wanaojifungua na wagonjwa pale wanapofanyiwa upasuaji kwenye hospitali zetu wanahitaji kuongezewa damu kwahiyo jambo hili ni la kiungwana, kizalendo na kihimani.”

Amesisitiza kuwa jambo hilo lililofanywa na wanahabari hao kwa kiasi kikubwa limeonyesha mfano mkubwa kwao na kwa wanajamii kwa ujumla lakini pia makundi mbalimbali kwenye Jamii kuona kwamba wana kila sababu ya kufanya mambo kama hayo ya kuchangia damu kwa ajili ya kuoka afya za watanzani hao.

Katibu Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), Bryson Mshana amesema katika kuadhimisha miaka hiyo 30 ya Uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu, Mkoa wa Mtwara wameamua kufanya zoezi hilo la kuchangaia damu ili kusaidia kuboresha hifadhi ya damu katika hospitali zao mbalimbali zilizopo ndani na nje ya Mkoa huo.

‘’Tumeona umuhimu kuadhimisha maadhimisho haya kufanya zoezi hili la kuchangiaa damu sisi waandishi wa habari kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali Mkoa huu wa Mtwara kama vile Serikali ya Mkoa wetu na makundi mengine kwa pamoja kushiriki zoezi hili la kuchangia damu kutokana suala la damu lina muhusu kila Mtu katika suala zima la afya na tunashukuru limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana ’’,

 

Kwa upande wao baadhi ya wanahabari hao akiwemo Florence Sanawa ambaye pia ni mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mwananchi akiwa miongoni mwa wachagiaji wa damu ‘’ Nimejitolewa kuchangai damu ili kusaidia wale wenye uhitaji wa damu na damu inaokoa maisha ya Watu wengi sana kama vile watoto wachanga, akina mama wajawazito wakati wa kujifungua’’,

Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Kusini, Dk Baraka Kandonga amesema katika Mkoa huo hali ya damu zipo lakini mahitaji kila siku bado yapo kwasababu kuna wagonjwa ambao wanahitaji damu na mapaka sasa awameshakusanya zaidi ya asilimia 98.

Hata hivyo bado mahitaji ya damu yapo kwasababu haiwezi kukaa kwa muda wa mwaka mzima na badala yake inakaa ndani ya siku 35 tu inakuwa imeshamaliza siku zake pia haiwezi kukaa ndani ya siku hizo 35 kwasababu ikishachangishwa inaenda kupimwa kisha inaenda kwa ajili ya matumizi hivyo wahitaji wa damu ni wengi kuliko idadi ya damu zinazokusanywa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x