Waanzisha mfuko maalum kujikwamua kiuchumi

KIKUNDI cha wadau eneo la Madale jijini Dar es Salaam, kimezindua mfuko maalum ‘Saccos’ wenye lengo la kuondoa utaratibu wa kuchangiana wanapokutana na changamoto pamoja na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika uzinduzi wa mfuko huo Disemba 9, 2023 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wadau Group, Stephen Kazimoto amewataka wanachama wa wadau kushiriki kikamilifu shughuli zinazoandaliwa na viongozi ili kukuza maendeleo ya umoja wao.

Kazimoto amesema kwa mwaka utakaoanza 2024 hawatopenda usumbufu kila mwanachama anapaswa ajitambue ili kuzidi kusonga mbele.

“Tangu kuanzisha kwa umoja huu wa wadau mwaka 2014 hadi sasa kikundi kimesimama kwasababu ya sisi viongozi kutenda haki kwa kila mmoja anapopata shida”, amesema Kazimoto.

Ameeleza kuwa walijenga kituo cha polisi ambacho kinasimamiwa na mzee Mponja ambapo walitumia fedha za wanakikundi Sh milioni 250, kituo hicho ujenzi haujakamilika hivyo amewaomba wanakikundi wenzie kufanya jitihada ili waweze kikimalizia.

Ofisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni, Zahara Kamtande amesema Saccos ni miongoni mwa vyama vya ushirika ambavyo vinajiunga kwa hiari ili kujikwamua kiuchumi.


Amesema Ushirika unaendeshwa na sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013,namba ya uendeshaji wa vyama vya ushirika umefanana karibia nchi nzima ila ushirika wa akiba na mikopo upo tofauti na vyama vingine.

“Kwenye ushirika wa akiba na mikopo kunasheria iliyoongezwa ambayo ni sheria ya huduma ndogo za fedha namba 10 ya mwaka 2018 hii sheria inaelezea namna ambavyo vyama vya ushirika wa akiba na mikopo inavyoshindana na taasisi zingine za fedha ambayo inasimamiwa na kanuni ya huduma ndogo ya fedha ya mwaka 2019”,

Ameeleza kuwa ili Sacoss yoyote iweze kujiendesha ni lazima kuwepo na kiingilio ambacho kitasaidia kujenga mtaji wa chama na mwanachama akilipia kiingilio na akataka kujiondoa fedha hiyo hairudishwi.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button