Waasi wa M23 wateka Minova na kuhatarisha Goma

CONGO : KUNDI la waasi wa M23 limeutwaa mji wa Minova, ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambao ni njia muhimu ya usambazaji kuelekea mji mkuu wa jimbo la Goma.

Jeshi la Congo limekiri kuwa vikosi vya waasi wa M23 vimesonga mbele, wakiwa wameuteka kitovu cha biashara cha Goma.

Msemaji wa jeshi la Congo, Sylvain Ekenge, amesema waasi wa M23 wamepiga hatua katika maeneo ya Bweremana huko Kivu Kaskazini na Minova huko Kivu Kusini.

Advertisement

Uvamizi wa Minova unaleta athari kubwa kwa mji wa Goma, huku mzozo ukiendelea kudhoofisha mji mkuu wa mkoa. SOMA: Mapigano yameanza upya Congo

Umoja wa Mataifa umebaini kuwa zaidi ya watu 230,000 wamekimbia kutokana na ghasia zinazozidi kutanda mashariki mwa DRC tangu Januari 1 mwaka huu.