Wabunge upinzani kumshtaki Rais Yoon Suk

KOREA KUSINI : WABUNGE wa upinzani nchini Korea Kusini wamesema watapiga kura ya kumfungulia mashtaka Rais Yoon Suk Yeol kwa kutangaza sheria ya kijeshi.

Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi anayeshtumiwa kumshauri rais huyo juu ya kutangaza sheria ya kijeshi kujiuzulu.

Awali, mbunge wa chama hicho cha Democratic, Kim Seung-won, aliliambia bunge kuwa tangazo hilo liliwachanganya  wananchi .

Advertisement

Chama tawala cha Yoon cha People Power Party kwa sasa kimegawanyika kuhusu mgogoro huo na kusema kitaunga mkono kura hiyo. SOMA: Wabunge 108 wampinga Rais Yoon Suk

Chama cha Democratic kinahitaji angalau wabunge wanane kati ya 108 wa chama tawala kuunga mkono hoja hiyo ili ipitishwe na theluthi mbili ya wingi wa kura za bunge hilo lenye viti 300.