DODOMA: Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, leo Februari 12, 2025, wamepatiwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Utoaji Huduma wa PSSSF Kidijitali.
Mafunzo hayo yalifanyika kwenye majengo ya Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Ridhiwani Kikwete.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru, amesema wataendelea kutoa mafunzo hatua kwa hatua ya kutumia mfumo huu wa kidigitali kwa kutumia simu janja kwa wanachama wake.
Kikwete alisisitiza kuwa mfumo huu, uliozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, unamuwezesha kila mwanachama kujihudumia mwenyewe wakati wowote na mahali popote.