BAADA ya kilio cha muda mrefu cha wanamichezo kuhusiana na Bima ya Afya, Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara, Benki ya NBC inatarajia kuwakatia bima wachezaji na familia zao.
Akizungumza na wanahabari leo Mei 3, 2023, Mkuu wa Masoko, David Raymond amesema bima hiyo ni kwaajili ya wachezaji wa waligi hiyo hata vilabu vingine vilivyo katika mfumo rasmi ambapo wachezaji watajiunga kupitia klabu zao.
Amesema bima hiyo itaweza kumsaidia mchezaji pamoja na familia yake ya watoto wake watatu.
“Mwanamichezo akipata tatizo akiwa katika mchezo, Nbc Bima itakuwa ikitoa fedha kiasi kwaajili ya kumpa pole wanafamilia ya kumsaidia kimaisha kwa kipindi hicho” alisema Raymond.
Raymond alisema lakini pia wamezindua kampeni ya Shinda Mechi Zako na NBC yenye malengo ya kuimarisha ustawi wa kifedha wa wateja na kusaidia juhudi za serikali katika kutoa huduma za kifedha na kukuza uchumi wa watanzania.
“Tuna furaha kuzindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako na NBC’, ambayo ipo kwa ajili ya kuwapa nguvu wateja wetu na kuwasaidia kufikia malengo yao ya kifedha kwa kuongeza thamani na uzoefu wao wa benki.
Kampeni hii itawapa wateja wetu huduma za KIbenki zenye gharama nafuu na rahisi, na pia kusaidia kukuza uchumi wao.”
Mkuu wa bidhaa za NBC, Abel Kaseko alisema Kupitia kampeni hiyo NBC imetumia baadhi ya wachezaji nyota wa Ligi Kuu ya NBC, Kupitia kampeni hiyo, wateja wataweza kunufaika na gharama nafuu za miamala kama vile kuweka standing order bure kabisa.
kulipia kwa kadi huduma za mtandaoni kwa punguzo la bei, na upatikanaji wa mikopo binafsi na ya biashara hadi milioni 150 ndani ya masaa 48.
“Wateja wanaweza kupata faida ya hadi asilimia 7% kwenye akaunti zao za NBC Malengo. Wateja pia wanaweza kupata mkopo wa kumalizia nyumba kwa gharama nafuu ili kukamilisha ndoto zao za ujenzi wa nyumba” alisema
Alimaizia kwa kusema Kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wa kada mbali mbali, Benki ya NBC imepanga kuwasaidia kutatua changamoto hizo kupitia ushauri na huduma za kifedha ambazo ni suluhisho za changamoito hizo