Wachimbaji haramu maeneo ya maji waonywa

TANGA: MKUU wa Mkoa waTanga, Dk Batlida Burian amepiga maarufu shughuli za uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu katika vyanzo vya maji vya mto zigi vilivyopo kata ya Amani wilayani Muheza.
Sambamba na hayo ameagiza Serikali ya Wilaya ya Muheza kuunda kikosi kazi maalumu ambacho kitakwenda kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi kando kando ya vyanzo hivyo elimu ya mazingira na madhara ya uharibifu unaofanywa kutokana na shughuli za kibinadamu.
Maagizo hayo aliyatoa wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujione uharibifu uliofanywa kwenye vyanzo hivyo uliofanywa na wachimbaji haramu wa madini ya dhahabu kwenye Wilaya ya Muheza.
Alisema kuwa Mto Zigi maji yake yanategemewa na wakazi wa Wilaya za Tanga, na Muheza hivyo uharibifu unaendelea hatua za haraka zisipochukuliwa athari yake inaweza kuwa kubwa zaidi.
“Kwa sasa Mamlaka ya Maji Tanga UWASA inatekeleza mradi mkubwa wa maji wa Hatifungani ya kijani hivyo iwapo kama hatutadhibiti uharibifu mradi huo hautaweza kutekelezwa lakini na wananchi wataweza kukosa huduma ya maji safi na salama,”amesema RC Batlida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Tanga Uwasa, Dk Ali Fungo amesema kuwa tayari wameweza kutumia kiasi cha Sh mil 820 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya utunzaji wa mazingira kwenye vijiji 34 ambavyo vinazunguka vyanzo hivyo.
“Hivyo iwapo serikali haitaweza kuchukuwa jitihada za haraka katika kuunga mkono jitihada hizo ustawi wa watu wetu utakuwa hatarini lakini na huduma ya maji itaweza kukosekana”alisema Dkt Fungo
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com