Wadau kujadili changamoto wachimbaji wadogo madini

ZAIDI ya wadau 700 wa madini, viwanda na taasisi za kifedha kesho wanatarajiwa kushiriki mkutano wa kwanza jijini Dar es Salaam, ili kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta suluhu kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Pia katika mkutano huo mkakati mpya wa kutoa elimu kwa wachimbaji wa wadogo wa madini nchi nzima utazinduliwa, ambapo  kila mchimbaji atafikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk Venance Mwasse, amesema mkutano huo utafanyika kwa siku mbili Aprili 5- 6, 2023 jijini Dar es Salaam, ambapo wanatutanisha wachimbaji wadogo wa madini ya viwandani pamoja na wenye viwanda wanaotumia madini na taasisi za kifedha kwa ajili ya kuwaelimisha kutafuta fursa za mikopo.

“Tutaendelea kwa kufuata aina ya madini, ili kumfikia kila mchimbaji kwa umuhimu ule ule kuliko kufanya mkutano kwa wadau wote wanaochimba madini, tunataka changamoto mahususi zinazowakumba kwahiyo tunaanza hapa madini ya viwandani na baadae tutaenda madini ya chumvi na mkaa,” amesema.

Amesema wanawaunganisha kujua changamoto kwa nini viwanda vya Tanzania vinatumia malighafi kutoka wakati zipo hapa nchini na kuna ajenda ya viwanda.

“Tunataka rasilimali zetu kuvunwa vizuri tumewaita wadau wengine kama wanaojihusisha na maabara kama viwanda vina changamoto za ubora basi tujue na maabara watoe suluhu hapo,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button