Wadau wajadili maendeleo mradi wa RISE

TIMU ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia (WB), Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Menejimenti ya Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na timu ya kusimamia mradi wa RISE leo Oktoba 16, 2025 wamekutana na kujadiliana kuhusu maendeleo ya mradi wa RISE (Mid-Term Review) katika jijini Dodoma.
SOMA: Sh bilioni 822 kuboresha Barabara vijijini
Kikao hicho kilichoongozwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff na kwa upande wa Benki ya Dunia iliongozwa na Mhandisi Sofia Guerrero Gamez.
Kikao hicho ni muendelezo baada ya timu ya mradi wa RISE Benki ya Dunia na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kutembelea maeneo ya mradi na kukagua maendeleo yake na kujionea kazi kubwa iliyofanyika katika mikoa ya Iringa, Lindi na Tanga.



