Wafanya jambo kunogesha Euro
DAR ES SALAAM: Wakati fainali za Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’, zikitarajia kuanza mwezi ujao, kampuni za Tigo, Parimatch, na Hisense zimezindua promosheni kwa michuano hiyo. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Kampuni hizo zimezindua promosheni ya “Zigo la Euro Cup na Hisense”, ili kuleta msisimko wa Kombe la Euro 2024 litakalo fanyika nchini Ujerumani.
Promosheni hiyo inaleta fursa za kipekee kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania ambapo timu 24 zitachuana katika miji 10 nchini Ujerumani,.
“Kombe la Euro si tukio la kimichezo tu; ni jambo la kimataifa ambalo linaunganisha mamilioni ya mashabiki wa soka duniani kote,” amesema Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa.
Kupitia ushirikiano huu, wateja watapata nafasi ya kushiriki katika droo za kuvutia za kushinda tiketi za kwenda Ujerumani kutazama mechi za Euro Cup moja kwa moja, pamoja na zawadi nyinginezo kama vile vifaa vya elektroniki kutoka Hisense.