Wafanyabiashara Afrika Kusini watafuta fursa za uwekezaji madini

TANZANIA imepokea wafanyabiashara wa madini zaidi ya 30 kutoka nchini Afrika Kusini wanaotafuta fursa za uwekezaji katika sekta hiyo.

Hatua hiyo imekuja siku chache, tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye ziara nchini Afrika Kusini na kuwaita wawekezaji kuja kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Rais Samia alitoa mwaliko huo alipokuwa katika ziara ya kiserikali ya siku moja ambapo pia alifanya mazungumzo  na Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina wa Madini Dk Abdulrahman Mwanga, amesema wafanyabiashara hao wameoneshwa fursa mbalimbali wanazoweza kuzitumia, ikiwemo ununuzi na usambazaji wa mitambo na vifaa mbalimbali kwa ambao hawatataka kujihusisha na uchimbaji.

“Tumezungumzia masuala ya uchimbaji madini kama fursa, utafitaji madini, ununuzi na usambazaji  wa bidhaa mbalimbali katika maeneo ya migodi kwa wale ambao hawahitaji kuwekeza moja kwa moja kwenye uchimbaji madini,”amesema Dk Mwanga.

Amesema uwekezaji katika sekta ya madini unazidi kuimarika na sasa ukuaji wake umefikia asilimia 7.

9, huku malengo yakiwa ni kufikia asilimia 10 mwaka 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na maendeleo kutoka South African Oil and Gas Alliance, Reelof Van Tonder amesema baada ya ziara ya Rais Samia Hassan waliwahamasisha jumuiya ya wafanyabiashara kuja nchi kutafuta fursa biashara ili waweze kuwekeza nchini.

“Tumekuja kuangalia fursa za biashara, tuna furaha kwa kupokelewa vizuri na wizara na kuelezwa taratibu za uwekezaji na vitu tunavyotakiwa kufanya au fursa nyingine ambazo tunaweza kuzitumia katika uwekezaji ndani ya sekta ya madini,”amesema

Habari Zifananazo

Back to top button