Wawekezaji Rorya waongoza harambee ukarabati madarasa

BAADHI ya wafanyabiashara na wawekezaji katika maeneo mbalimbali wilayani Rorya mkoani Mara wameanzisha mkakati wa kukarabati wa madarasa na upanuzi wa shule za msingi walizosoma kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan aliyelenga kuboresha sekta ya elimu.

Wawekezaji watano waliowekeza katika mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mara wakiongozwa na mfanyabiashara wa mazao mkoani Kigoma Hunga Marwa akiambatana na wafanyabiashara wengine wameendesha harambee na kufanikiwa kukusanya fedha zaidi ya Sh milioni 45.

Harambee hiyo imeenda sambamba na mifuko ya saruji zaidi 120 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Erengo inayokabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwemo ukosefu wa jengo la utawala.

 

Wafanyabishara wengine ni Daud, Aloyce, Nyantora Mwita Chacha, muwekezaji wa kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti Rorya na mlezi wa vijana Mkoa wa Mara Wilfred Nyihita, Muwekezaji mkubwa jijini Mwanza, Joseph Magige maarufu Tajiri Mtoto na mfanyabiahara wa Mwanza Robert Msilikale.

Harambee hiyo iliyohudhuliwa na viongozi wa madhehebu ya dini ,wanasiasa,wakulima na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ikiwa ni mwendelezo wa harambee ya uboreshaji wa shule za msingi.

Zoezi hilo limeanza shule ya msingi Bitirya, ikifuatiwa na Kyabaigi na Erengo ambayo imetengewa fedha kutoka ofisi ya Rais kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya kisasa, majengo na nyumba za walimu.

Habari Zifananazo

Back to top button