Wafanyakazi TCAA washiriki UDSM Marathon

WAFANYAKAZI 70 wa Mamlaka ya Anga (TCAA) wameshiriki mashindano ya riadha ya UDSM Marathon kwa lengo la kuweka vyema afya zao kama sehemu ya mazoezi kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na pia kudumisha ushirikiano.

Hayo yamesemwa na Teophory Mbilinyi, ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za mamlaka TCAA leo Desemba  3,2023 wakati waliposhiriki mbio hizo jijini Dar es Salaam.

Amesema mazoezi yanasaidia wafanyakazi kuwa imara zaidi kiafya, hivyo kuongeza ufanisi katika kutekeleza  majukumu yao.

Advertisement

Kwa upande wake Jackline Ngoda mfanyakazi wa TCAA amesema mbio hizo ni muhimu kwao na ndiyo sababu wameshiriki kwa wingi.

Mgeni rasmi katika mbio hizo alikuwa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, ambapo kaulimbiu ilikuwa ni Kimbia Nasi Boresha Maisha ya Wanachuo

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *