Wafanyakazi USAID wasimamishwa kazi

MAREKANI : SHIRIKA la msaada wa kibinadamu la Marekani USAID limetangaza kuwapumzisha kazi kwa muda wafanyakazi wake dunia nzima ikiwemo wale walioko nchini Marekani, kuanzia Februari 7.
USAID imeeleza kuwa wafanyakazi wake walioko nje watarudishwa nyumbani, ingawa pia limesema hatua hiyo haitowagusa wafanyakazi wenye majukumu maalum.
Uamuzi huo ni sehemu ya ya mageuzi ya serikali ya Marekani inayoongozwa na Donald Trump na bilionea Elon Musk ya kutaka kupunguza matumizi na imesababisha hasira na upinzani mkubwa kutoka chama cha Democratic na jumuiya ya mashirika ya haki za binadamu.
USAID ni shirika la msaada la Marekani linalofadhili miradi kiafya na masuala ya dharura katika mataifa 120 duniani ikiwemo mataifa masikini kabisa ya ulimwengu.


