Wageni Vietnam watembelea Mahakama Tz

DAR ES SALAAM: WAGENI mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Afrika wameridhishwa na hatua za ukuaji wa maendeleo ya teknolojia ya Tehama katika Mahakama ya Tanzania.

Viongozi 18 wa Chama cha Kicomunist kutoka nchini Vietnam ni miongoni mwa waliotembelea Mahakama ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia cha Temeke ili kuangalia utendaji kazi ambapo kupitia kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, PHA Dunh Track amesema imekuwa mfano bora katika ukuaji na matumizi ya teknolojia ya Tehama hali iliyowafanya kutembelea.

Advertisement

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema ujio chama hicho ni muendelezo wa wageni kutoka ndani na nje ya Afrika ambapo mwezi ujao ugeni kutoka Mahakama ya Kazakstan watatambelea Tanzania huku akisisita nchi ya Tanzania kuendelea kuwekeza katika Tehama.

SOMA: Wadau wa mahakama wahamasishwa mfumo wa kidigitali

“Maboresho yeyote mara nyingi watu wanayaogopa mabadiliko kwa hiyo wananchi kuamini kwamba haya maboresho ni ya kweli wanaona kama ni ya muda na kuwa tayari kuyatumia wapo wananchi ambao walishaelezwa sio mara moja sio mara kumi wara 20 kwamba huna haja ya kuja mahakamani kufungua Shauri unaweza ukafungua shauri ukiwa shambani au popote,”

“Mabadiliko ya kiteknolojia yanatuhijati tuwafundishe watalaamu wetu kwaiyo kila wakati inabidi tuwanoe wataalamu wetu waweze kuendana na kasi hii na uhakika ni kwamba faida ya maboresho ya teknolojia ni makubwa kuliko hasara ya kutoboresha,”amesema Elisante.

SOMA: Bil 5/- zaokolewa usuluhishi Mahakama Kuu miezi mitatu

Aidha Prof. Elisante amesema moja ya changamoto kubwa kwa sasa ni uelewa wa Watanzania kuhusu mifumo ya Tehama katika mahakama huku akisisitiza mahakama kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya mifumo hiyo katika shughuli za mahakama.