DAR ES SALAAM; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewataka wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania kuendelea kutimiza malengo kwa kuzingatia maadili, nidhamu na uaminifu katika kufanya kazi na kukuza taaluma nchini.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wahasibu na wakaguzi zaidi ya 2000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wamekutana kujadili mambo mbalimbali yanayohusu taaluma yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Sylivia Temu, amesema kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye somo la hesabu wanaohitimu kidato cha nne kunasababisha kudhoofisha fani hiyo kwa kukosekana kwa wahasibu wapya.
“Kukua kwa fani kunategemea zaidi wanafunzi wanaohitimu, hivyo kutofanya vizuri kwenye somo la hesabu kunazidi kuzoretesha fani yetu, hivyo ni vyema serikali kupitia wizara ya elimu kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo,” Prof. Sylivia Temu.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno, amesema matumizi ya Tehama yanatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa wahasibu nchini ili kuendana na kasi ya utendaji kidigitali.
Comments are closed.