Wahujumu ugawaji pembejeo kukamatwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kuwachukulia hatua watendaji wa kata na vijiji ambao wanahusika kuhujumu ugawaji wa pembejeo.

Watendaji hao ni pamoja na maafisa kilimo wanaoiba na kuhujumu ugawaaji wa pembejeo za ruzuku ambazo zimetolewa na serikali kwa wakulima wa korosho nchini.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Agosti 13 wilayani Tandahimba na kusema suala ugawaji wa pembejeo katika Wilaya ya Tandahimba imekuwa biashara ya wachache walioko madarakani.

“Suala la mkulima lichukuliwe serious, ni suala ambalo Raisi aliweka mpaka ruzuku ya bilioni hamsini ili pembejeo zitoshe na ni muhimu zikatosha,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema hayo baada ya wakulima kulalamikia watendaji na viongozi ngazi ya kata na vijiji wakiwemo maafisa kilimo kuwahujumu wakulima pembejeo huku wengine wakinyimwa licha ya kujisajili kupata pembejeo hizo.

Amemtaka DC wa Tandahimba kukaa na Chama kikuu Cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) kutatua kero na mnalalamiko ya wakulima kuhusu ugawaji wa pembejeo za ruzuku.

Majaliwa amesema serikali ilishatoa majibu ya kero kubwa kwa wakulima ikiwemo upatikanaji wa pembejeo za zao la korosho.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button