Wahusishwa kushawishi wanawake kwenda Msomera

WANAHARAKATI wamehusishwa na vitendo vya kuwashawishi wanawake kuwakataa waume zao waliojiandikisha kwa hiari kutoka Ngorongoro kwenda Msomera wilayani Handeni na kupelekea baadhi ya wanaume kubaki wapweke.

Akizungumzana wanahabari, Mzee Kidori Tarabeta mkazi wa Olpiro, Eyasi wilayani Ngorongoro anasema yeye ameamua kuhama kwa hiari kwa kuwa amechoka kuishi kwa shida na mateso makubwa.

Amesema ameamua kuhama kwa hiari licha ya kuwa kwenye matatizo makubwa na mkewe ambaye ameshawishiwa kutohama ili hali awali alikuwa mstari wa mbele kuhama na kuondoka ndani ua eneo hilo.

“Mke wangu aliondoka na watoto watatu na amerudisha mtoto mmoja akiwa maiti(amefariki), nimekaa kimya na wanaendelea kumshawishi asihame kwa kuwa mamlaka hawezi kumuhamisha mtu au familia yenye mgogoro.”

Tarabeta anasema yeye na familia yake wako tayari kuhama lakini amekwama kuondoka ndani ya hifadhi kutokana na mkewe kukataa kuondoka siku ambayo wameitwa kujiandaa na safari ya kwenda Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Kunawanaharakati wanawashawishi wanawake wawakatae waume zao au kuondoka na watoto ili tu kuzuia tusiende Msomera yani baada ya kukataa aliondoka na watoto wake watatu na kwenda nao kijijini kwao Samburai na kumshawishi asiondoke kijijini hapo na kumfanya kuendelea kuishi kwa shida kubwa kutokana na kutegemea ulinzi na vibarua kwa watu mbalimbali.

“Sisi ndio watafutafutaji, tunapaswa kusikilizwa na sasa tumepata fursa lakini wanawake wanatukomesha na wanatumia fursa hiyo ili tusihame baada ya kushawishia tusihame,Jambo ambalo sio zuri”

Hivyo anaiomba serikali isiwasikilize wanawake wanaowakomesha wakati wao ndio watafutaji na wapo mstari wa mbele katika kuleta maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button