Waislamu washauriwa kutumia Ashura kupinga ukatili

TANGA: Waislamu nchini wametakiwa kuitumia siku ya Ashura kupinga na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii.
Mkuu wa Utawala wa Taasisi ya Bilal Muslim Mkoa waTanga, Sheikh Abdulrazak Bilal amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye ni Imamu Hussein (AS).
Amesema kuwa Imamu Hussein ni kielelezo cha kiongozi ambaye alikufa kwa ajili ya kutetea usawa miongoni mwa jamii kwa kupinga vitendo viovu hivyo ni muhimu Waislamu nchini nao wakawa mfano bora wa kutetea vitendo vya kidhalimu.
“Ni wajibu wetu waislamu kuitumia siku ya Ashura kama kielezo cha kupinga vitendo viovu lakini na kuhamasisha matendo mema miongoni mwa jamii ili dunia iweze kubaki mahali salama,” amesema Shekhe Bilal.