Waislamu watoa wito kudumisha maadili

DAR ES SALAAM: WAUMINI wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuishi kwa kuzingatia maadili mema waliyojifunza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa kudumisha matendo mema na kujiepusha na maovu katika maisha yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa leo na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omari, alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la watoto yatima na wenye mahitaji maalum lijulikanalo kama Mama Samia Orphans Eid Day Out, lililofanyika katika viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Shekhe Omari amesema Ramadhani ni kipindi muhimu kinachowakumbusha Waislamu namna bora ya kuishi kwa kufanya mema na kuacha maovu.
“Waislamu wanatakiwa kuishi kama walivyokuwa wanaishi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni mwezi unaotufundisha kufanya mema na kujiepusha na maovu,” amesema Omari.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kusaidiana, kusameheana, pamoja na kuendeleza ibada usiku na mchana kama ilivyokuwa wakati wa mfungo huo.
Katika hatua nyingine, Shekhe Omari ameipongeza Kampuni ya Chocolate Princess kwa kuandaa tamasha hilo la kiimani, akieleza kuwa ni mfano mzuri wa kuwajali na kuwathamini watoto wenye mahitaji maalum, hususan yatima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Limited, Mboni Masimba, amesema kampuni yake imekuwa ikitoa misaada kwa watoto yatima kwa muda mrefu, na kwamba tamasha hilo limeandaliwa kufuatia uzoefu wake wa shughuli za kufuturisha.
Amesema tamasha hilo limewakutanisha zaidi ya watoto 1,000 kutoka vituo 13 tofauti, lengo likiwa ni kuwapa furaha na kuwajenga kiimani.

Masimba amewahimiza watoto hao kuwaheshimu walezi wao, akibainisha kuwa heshima na utiifu vitawasaidia kupata baraka na mafanikio katika maisha yao, sambamba na kuzingatia ibada.



JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com