Waitara NBC Trophy yavuta wachezaji 147

MWENYEKITI wa Klabu ya Gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo, amesema shindano la Waitara NBC Trophy limepata mafanikio baada ya kuvutia wachezaji 147 kujitokeza kushiriki katika vipengele tofauti.

Amesema kivutio kikubwa zaidi katika shindano hilo ni mshindi wa jumla Dk Edmund Mndolwa ambaye ana umri mkubwa ukilinganisha na washiriki wengine.

Advertisement

Luwongo amesema shindano hilo la kumuenzi Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara, lilikuwa lifanyike mwaka jana lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hawakufanikiwa na ndio lilifanyika mwishoni mwa wiki, huku akitangaza lingine litafanyika tena hapo baadaye.

“Tumepata mafanikio kwa sababu washiriki wamekuwa wengi katika vipengele lakini mwisho wa siku washindi ni wachache, tunawapongeza wote walioshiriki wakiwemo watoto, vijana, wanawake na wazee,”amesema.

Jenerali Waitara ni muasisi wa klabu ya Gofu ya Lugalo na ndiye aliyeanzisha Viwanja vya kuchezea Gofu vya Lugalo, hivyo wamekuwa wakimuenzi kwa shindano kila mwaka kuthamini mchango wake katika michezo nchini.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *