Wajasiriamali 30 wanufaika na mitungi ya gesi Dar

KAMPUNI Udhamini wa mchezo wa ndodi ya Mafia imegawa mitungi ya gesi kwa mama lishe eneo la Magomeni Sokoni jijini Dar es Salaam kumuunga mkono kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondokana matumizi ya nishati chafu.

Mama lishe hao zaidi ya 30, wamepatiwa mitungi hiyo wakati wa kuwatambulisha mabondia 14 watakaopanda ulingoni leo kwenye shindano la Knockout ya Mama.

Akizungumza baada kugawa mitungi hiyo Mkurugenzi wa Mafia, Ally Zayumba, amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanaunga mkono kampeni ya Rais Samia ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu kwa watanzania.

“Rais wetu, Dk Samia amekuwa akihamasisha watanzania kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo ni mkaa na kuni, nasi tukaona hatuna budi kuunga mkono jitihada hizo kwa kugawa mitungi kwa Mama lishe wenye mahitaji katika soko hili la Magomeni,” amesema.

Baadhi ya Mama lishe waliopata mitungi hiyo wameishukuru kampeni ya Mafia wakisema itawasaidia kupika kwa haraka na kwa muda mfupi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button