“Wajibu wa serikali waandishi kuwa salama”

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha kipindi chote cha machakato wa uchaguzi, waandishi wa habari wanakuwa salama.
Dk Biteko amesema serikali itaendelea kulisimamia hilo kwa nguvu zetu zote. Amesema waandishi wa habari wanatakiwa kuwa walinzi wa kweli, wajenzi wa amani.
“Ni wajibu wenu pia kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinabaki kuwa kioo safi cha jamii kisichokuwa na doa wala uzushi, chuki wala upendeleo ,”amesema Dk Biteko.



