Wajumbe jukwaa la ushindani wapewa maagizo

DAR ES SALAAM: WAJUMBE wa Baraza la Ushindani Afrika wametakiwa kuja na suluhisho la kupata bidhaa bora kwa bei nafuu kupitia ushindani wa haki na kuleta faida kwa wananchi.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo alipozungumza na waandishi wa habari katika jukwaa la Ushindani Afrika lililofanyika jana Aprili 13, 2026 Dar es Salaam.

Londo amesema nchi za Afrika zinapaswa kuweka wazi sera zao za ushindani ili kuweka mazingira wezeshi ya biashara pia kuchochea mapinduzi ya viwanda.
Amesisitiza kuwa kwa namna Afrika inavyoendelea kuunganishwa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ipo haja ya kuwa na sera za ushindani zenye mshikamano.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kujitanua kukuza utamaduni wa ushindani ili kufikia Dira ya Taifa 2050.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani (FCC), Hadija Ngasongwa amesema jukwaa hilo ni madhubuti kwa lengo la kushirikiana kujengeana uwezo.

Amesema jukwaa hilo ACF linaloshirikisha nchi wanachama 37 pia lina lengo la kurahisisha utatuzo wa pamoja na kudhibiti ushindani wa haki.





thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. ng.yandaz.com