Wakazi wa Itwangi wajitokeza msaada wa kisheria

SHINYANGA: WAKAZI wa jimbo la Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamejitokeza kupata msaada wa kisheria katika kampeni ya awamu ya pili ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid huku wakipongeza kupata msaada wa kirafiki usioendelea kuleta mgogoro.
Wakizungumza baada ya kupata msaada wa kisheria leo kupitia elimu inayotolewa Kata ya Didia, mkazi wa kata hiyo, Mponeja John aliyefika kwa madai ya kudhulumiwa eneo lake pembeni mwa nyumba anayoishi alieleza kufika kwenye Baraza la Kata la Ardhi na nyumba lakini hakupata msaada wowote.

John amesema mtu aliyechukua eneo lake alimfikisha kuanzia ngazi ya kijiji hadi baraza la kata uamuzi uliokuwa ukitolewa hakuridhika nao na kushindwa kufungua kesi kwa madai yakutakiwa kutoa shilingi 500,000 kuendesha kesi hiyo ngazi ya wilaya.
“Baraza la ardhi halijanisaidia limekuwa likinizungusha nikijaribu kusema niende ngazi ya wilaya inatakiwa niweke mwanasheria ambaye alidai nimpatie laki tano ndiyo asimamie kesi yangu nikawa sina pesa leo msaada wa kisheria upo hapa nimepata kufarijika sana,” amesema John.

John amesema amefurahishwa na ushauri wa wataalamu wa msaada wa kisheria wakutaka shauri lilirudi kwenye baraza la ardhi upya na ikishindikana watampatia wakili wa serikali bure atakaye simama mahakamani.
Katibu wa baraza la ardhi kata ya Didia Engelbert Shoto aliyefika kwenye eneo la msaada wa kisheria ameeleza kufahamu mgogoro huo alikiri kutambua mgogoro huo huku akieleza baadhi ya wananchi kutojua sheria na wao kwenda kinyume nakuomba warudi tena upya kuutatua mgogoro huo naikishindikana watoe shauri la kusonga mbele.
Wakili wa serikali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Salehe Hassan amesema migogoro mingi ambayo wameipokea inahusu ardhi kinachosababishwa ni maeneo mengi kutokupimwa ,kupangwa na kumilikishwa kwani maeneo yaliyopimwa mipaka yake ipi vizuri kama haikupimwa ni ngumu kutambulika.
“Kweli huyu mwananchi amekuja na malalamiko yake lakini hana hati miliki ya eneo angekuwa nayo mgogoro usingeendelea ninaishauri serikali kupanga miji au maeneo na kumilikisha ardhi kwa ushauri uliopatikana tumeomba baraza la ardhi la kata lirudi upywa kuangalia namna ya kutatua mgogoro huo” amesema Hassan.



