PALESTINA : TAKRIBAN watu 12 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel, wengi wao wakiwa wakimbizi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika nyumba moja kaskazini mwa ukanda wa Gaza.
Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal amesema Wapalestina 10 wameuawa kufuatia shambulio la Israel lililolenga nyumba moja katika eneo la Beit Lahia.
Bassal ameongeza kuwa mtoto mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio lingine tofauti lililolenga nyumba karibu na eneo la Jabalia. SOMA : Israel yashtumiwa kuhusika mauaji halaiki Gaza
Zaidi ya miezi 14 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, Marekani imeeleza matumaini kuhusu uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ukanda wa Gaza.