Wakimbizi waliotoroka kambini kusakwa Kigoma

SERIKALI mkoani Kigoma imetangaza kuanza operesheni maalum ya kuwasaka wahamiaji haramu wakiwemo wakimbizi wa Burundi wanaodaiwa kukimbia makambini na kuishi mtaani kinyume cha sheria za uhamiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Simon Sirro amesema mkoa huo unakabiliwa na ongezeko la raia wa kigeni wanaoishi bila kufuata taratibu, hali inayodaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wakimbizi kutoka Burundi. Amesema operesheni hiyo itahusisha maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ikiwemo sehemu zinazohisiwa kuwa na vitendo vya uhalifu, wahalifu pamoja na wahamiaji haramu.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Sirro amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kurejesha utulivu na kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa. Awali Idara ya Uhamiaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilitangaza kufungwa kwa kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo ifikapo Machi 31 mwaka huu, ambapo wakimbizi waliokuwa wakiishi hapo wanatarajiwa kurejeshwa nchini kwao.

Hivi karibuni imeripotiwa kuwa baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakirejea Burundi, lakini wengine wanadaiwa kutoroka na kuendelea kuishi Kigoma bila kibali halali. Serikali imeeleza kuwa operesheni hiyo itafanyika nchi kavu na ziwani ili kudhibiti hali hiyo na kuondoa vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama na amani ya wananchi. SOMA: Serikali: Tutunze amani tusigeuke wakimbizi

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button