Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720

Wakulima zaidi ya 400 kunufaika fursa SBL

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720

Dodoma: Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imeitikia wito wa serikali wa kuboresha mazingira mazuri kwa wakulima wa ndani katika kununua mazao zaidi na kutanua mtandao kutoka kundi hilo.

Kampuni ya SBL tayari inatumia zaidi ya asilimia 70 ya nafaka kama mtama, mahindi na shayiri kutoka wakulima wa ndani zaidi ya 400.

Akizungumza katika kilele cha maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma, Afisa Kilimo Biashara wa SBL, Aloyce Kimaro alisema kampuni hiyo itaendelea kuwawezesha wakulima wetu kupitia elimu ya kilimo-biashara na msaada wa vifaa kama vile mbegu za bure.

SOMA: Diamond Platnumz kivutio SBL ikija kivingine

“Tunafanya kazi na wakulima wadogo hadi wakubwa tukiwapatia mikataba ili kuhakikishia soko la mazao yao. Zaidi ya hayo, ushirikiano wetu unajumuisha mikoa mingi, ikiwemo Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, na Nyanda za Juu Kusini.

Aliitaja mikoa 16 ambayo SBL inafanya kazi na wakulima kuwa ni Singida, Dodoma, Manyara, Moshi, Arusha, Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa, Kagera, Njombe, Ruvuma, Tabora, Mwanza, Mara na Tanga.”

Kimaro pia alitaja kuwa SBL imeweka mikakati ya kupanua uwezo wake wa kununua kutoka kwa wakulima wa mtama mwekundu, pamoja na wakulima wa mtama mweupe ambao tayari wananunua kutoka kwao katika mikoa hiyo.

SBL pia imeonyesha nia ya kuendelea kuwaunganisha wakulima wake na taasisi zinazotoa pembejeo na mikopo, ikitoa msaada wa kina zaidi ya kununua mazao yao tu.

Alisema lengo la SBL ni kuhakikisha wanatoa bidhaa za hali ya juu za kuanzia shambani ambapo huwatembelea wakulima na kutambua juhudi zao, kufanya uchunguzi wa udongo na kuwapa mbegu bora zaidi.

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720

Habari Zifananazo

Back to top button