DAR ES SALAAM; Idara ya Habari (Maelezo), imeandaa programu maalum ya kuwakutanisha Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote kwenye kila mkoa pamoja ili waeleze utekelezaji wa masuala mbalimbali katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini .
“Mikutano hiyo ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi itaanza Dodoma , Morogoro, Pwani na Dar es Salaam na Awamu ya pili ya Program hii itafanyika katika mikoa ya Manyara, Arusha, Tanga na Kilimanjaro,” amesema.